Keki ya Mugabe akiadhimisha miaka 92

Image caption Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, amekata keki kubwa na kuzima mishumaa kusherekea siku yake ya kuzaliwa

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, amekata keki kubwa na kuzima mishumaa kusherekea siku yake ya kuzaliwa.

Kiongozi huyo mkongwe muanzilishi wa taifa hilo lililoko Afrika ya Kusini ameadhimisha miaka 92 ya kuzaliwa kwake.

Keki hiyo ilikabidhiwa bwana Mugambe katika sherehe iliyoandaliwa na wafanyikazi wake asubuhi ya leo.

Image caption Keki hiyo ilikabidhiwa bwana Mugambe katika sherehe iliyoandaliwa na wafanyikazi wake asubuhi ya leo.

Maandishi ya keki hiyo yalikuwa ‘ siku njema ya kuzaliwa Gushungo’

Gushungo ni jina lake la ukoo.

Sherehe hiyo iiyoandaliwa kwenye ikulu ya rais ilihudhuriwa na majenerali wa kijeshi na wageni wengine mashuhuri walioalikwa.

Image caption Sherehe hiyo iiyoandaliwa kwenye ikulu ya rais ilihudhuriwa na majenerali wa kijeshi

Siku ya kuzaliwa kwake ilikuwa hapo jana na amepanga sherehe nyengine itakayo gharimu takriban dola milioni moja $1m huko Masvingo , Kusini mwa mkoa wa Zimbabwe, ripoti zinasema.