Aliyedaiwa kuiba mtoto Afrika Kusini akanusha mashtaka

mama Haki miliki ya picha AFP
Image caption Celeste Nurse, mwenye nguo nyekundu, anasema ndiye mama mzazi wa Zephany

Mwanamke aliyetuhumiwa kuiba mtoto wa umri wa siku mbili nchini Afrika Kusini mwaka 1997 amekanusha mashtaka mahakamani.

Polisi wanamtuhumu kwa kujifanya kuwa mamake mzazi wa msichana huyo na kuondoka naye kutoka hospitali maarufu sana mjini Cape Town.

Mwanamke huyo wa umri wa miaka 50 alikamatwa mwaka jana baada ya kumfikisha mtoto huyo aliyepewa jina Zephany Nurse, shuleni.

Celeste na Morne Nurse, wazazi wa msichana aliyefanana sana na msichana huyo shuleni walianza kushuku na wakawajulisha maafisa wa polisi.

Uchunguzi wa chembe nasaba ulithibitisha kwamba Zephany alikuwa mtoto wao, polisi walisema.

Amekuwa akiishi na mtuhumiwa, ambaye hawezi akatajwa jina lake kwa sababu za kisheria, karibu na nyumba ya Celeste na Morne Nurse katika mtaa wa Cape Flats, mjini Cape Town.

Zephany kwa sasa anatuzwa na shirika la kusaidia watoto.

Operesheni kubwa ya kumtafuta ilifanywa mwaka 1997 lakini hakupatikana.

Bi Nurse ameambia mahakama kwamba Zephany ni bintiye wa kwanza, na kwamba alikuwa na umri wa miaka 18 alipojaliwa mtoto huyo kwa njia ya upasuaji hospitali ya Groote Schuur.

Ni katika hospitali hiyo ambapo upasuaji wa kwanza wa kupandikiza kiungo duniani ulifanyika mwaka 1967.