Muuguzi wa Ebola Cafferky alazwa tena

Image caption Muuguzi Pauline Cafferkey

Muuguzi wa Scotland, Pauline Cafferkey, amelazwa kwa mara ya tatu baada ya kuambukizwa ugonjwa wa Ebola mwaka wa 2014.

Madaktari wa afya wamesema, muuguzi huyo mwenye umri wa miaka 39 yuko chini ya uchunguzi katika wodi maalum ya hospitali ya chuo kikuu cha Queen Elizabeth huko Glasgows.

Bi.Cafferkey kutoka kusini mwa Lanarkshire , alipata maambukizi ya Ebola nchini Sierra Leone.

Alitibiwa katika hospitali ya Royal Free mjini London, lakini alirudishwa mwezi Oktoba baada ya virusi vya Ebola kumsababishia ugonjwa wa uti wa mgongo.