Facebook kubaini maeneo ya wateja wake

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ramani ya facebook

Facebook imetangaza kuwa itatengeza na kutoa ramani zenye maelezo mengi kuhusu maeneo ambayo inaamini wateja wake wanaishi kwa uma baadaye mwaka huu.

Mtandao huo wa kijamii umekuwa ukitumia programu za kiintelijensia kutafuta picha za satelite ili kubaini mijengo ya binaadamu.

Inatumai kutumia ramani hizo kubaini pale ndege zisizo na rubani za mtandao zitawekwa ili kutuma maelezo.

Lakini pia imesema kuwa watu wengine pia wanaweza kutumia ramani hizo.

''Tunaamini kwamba data hii itakuwa na athari nyingi kama vile uchumi wa kijamii,utafiti pamoja na kutathmini hatari ya majanga,''ilisema facebook katika blogu.