Mtoto wa miaka 4 alihukumiwa kimakosa Misri

Image caption Kijana aliyehukiwa kimakosa

Mahakama moja ya kijeshi nchini Misri ilimuhukumu kwa makosa kijana mmoja wa miaka minne kifungo cha maisha jela kwa mauaji wiki iliopita,jeshi limekiri.

Msemaji wa jeshi Kanali Mohammed Samir amesema kuwa mahakama hiyo badala yake ingemshtaki na makosa kama hayo kijana mwenye umri wa miaka 16 mwenye jina kama hilo.

Ahmed Mansour Qurani Ali alipatikana na hatia pamoja na wengine 115 kuhusiana na ghasia zilizotekelezwa na wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood katika jimbo la Fayoum mwaka 2014.

Wakili wake aliwasilisha stakhabadhi akithibitisha alikuwa yeye wakati huo.

katika chapisho lililowekwa katika mtandao wa facebook kwa lugha ya kiarabu,Kanali Samir alisema kuwa Ahmed Mansour Qurani Sharar mwenye umri wa miaka 16 angehukumiwa na wala sio Ahmed Mansour Qurani Ali.

Haijulikani ni nini haswa kitakachompata kijana huyo wa miaka 4.

Wakili wa mtoto huyo alisema kuwa jina lale liliongezwa katika orodha ya washukiwa kwa makosa,na kwamba maafisa wa mahakama hawakupeleka kibali chake cha kuzaliwa kwa jaji ili kuthibitisha umri wake wakati wa kosa hilo.

Alihukumiwa na mashtaka manne ya mauaji,jaribio la mauji na kuharibu mali ya serikali.