Jaji wa korti ya juu Kenya asimamishwa kazi

Jaji
Image caption Jaji Philip Tunoi

Rais Uhuru Kenyatta amemsimamisha kazi jaji wa mahakama ya juu aliyetuhumiwa kuchukua hongo katika kesi kuhusu kuchaguliwa kwa gavana wa Nairobi.

Rais Kenyatta amemsimamisha kazi Jaji Phillip Tunoi na akateua jopo la kuchunguza madai dhidi yake, kwa mujibu wa mapendekezo ya Tume ya Huduma za Mahakama.

Jaji adaiwa kupokea rushwa ya $2m Kenya

Jopo la kumchunguza jaji huyo litaongozwa na Jaji Sharad Rao ambaye ndiye mwenyekiti wa Bodi ya Kuwachunguza Majaji na Mahakimu.

Haki miliki ya picha JMVB
Image caption Jaji Sharad Rao

Wanachama wengine wa jopo hilo ni Jaji Roselyn Korir, Jaji Mstaafu Jonathan Havelock, Judith Guserwa, James Kaberere Gachoka, Abdirashid Abdullahi Hussein na George Munji Wakukha.

Jaji Tunoi amekanusha madai dhidi yake.