Vazi la mwanamitindo wa Afrika lavaliwa na mcheza densi wa Beyonce

Haki miliki ya picha AP
Image caption Beyonce

Mwanamtindo wa Ivory Coast ,Loza Maleombho amejipatia sifa baada ya mtindo wake mmoja kuonekana kwenye kanda mpya ya video ya mwanamuziki nyota wa Marekani Beyonce.

Vazi hilo limevaliwa na mwanadensi katika video hiyo ya mwanamuziki huyo Marekani.

Bi. Maleombho alianza kazi yake ya mitindo huko mjini New York, lakini baadaye akahamia Ivory Coast.

Mitindo yake imeenea nchini Nigeria , Uingereza na Marekani.