Kylie Jenner:Sitaki maisha ya umaarufu

Image caption Kylie Jenner

Kylie Jenner ataka kustaafu na kuwa mfanyibiashara.

Kylie Jenner yuko tayari kustaafu, amesema kwenye mtandao wake wa Instagram.

Nyota huyo ambaye ndiye mdogo katika kipindi cha Keeping up with the Kardashians ameambia gazeti moja la Marekani kuwa uwepo wake mitandaoni umeathiri ukakamavu wake'

Jenner amesema ameangaziwa vya kutosha na sasa anataka kufanya kazi ambazo haonekani hadharani.

Amesema kuwa ana zaidi ya wafuasi milioni 52 katika mtandao wake wa Istangram na zaidi ya wengine milioni 14 katika mtandao wa twitter.

Haki miliki ya picha AP AND REUTERS
Image caption Babaake Kylie Jenner

Katika umri wake wa miaka 18 ameoneka kwa miaka tisa kwenye runinga na katika kanda za video za wanazamuziki kama vile Tyga na Jaden Smith.

Amewahi kuwa mwanamitindo katika runinga na amesema ndio kitu anachotaka.

'Nimekuwa hivyo kila siku . nataka kuwa mfanyibiashara na asiyejulikana. Kylie Jenner anastahili kustaafu''