Blaise Compaore sasa ni raia wa Ivory Coast

Blaise Compaore Haki miliki ya picha
Image caption Rais wa zamani wa Burkinafaso Blaise Compaore sasa ni raia wa Ivory Coast

Rais alieondolewa madarakani nchini Burkina Faso Blaise Compaore amepewa uraia wa Ivory coast , na hivyo kuondolewa kwa matarajio ya kurejeshwa nyumbani kukabiliana na mashtaka ya mauaji dhidi yake . Agizo la kumpatia uraia lilitolewa na rais Alassane Ouattara mnamo mwezi wa Novemba 2014, lakini amri hiyo imefahamika sasa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Blaise Compaore amekua uhamishoni Ivory coast tangu alipopinduliwa na jeshi mwaka 2014

Bwana Compaore anatafutwa kwa madai ya kuhusika katika mauaji ya kiongozi maarufu wa wa zamani wa Thomas Sankara mwaka 1987.

Utawala wake wa miaka 27 ulimalizika mwezi Octoba -2014 baada ya wimbi la maandamano ya upinzani.

Haki miliki ya picha
Image caption Blaise Compaore anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kiongozi wa zamani Thomas Sankara pichani

Bwana Compaore, ambae mkewe ni raia wa Ivory Coast, amekua uhamishoni nchini Ivory Coast tanga alipopinduliwa mwezi Octoba 2014.

Kibali cha kumkamata kilitolewa mwezi Desemba.

Bwana Sankara, aliekua na itikadi za mrengo wa kushoto alionekana kama "Che Guevara wa Afrika ", anaangaliwa na waafrika wengi kama shujaana alirithiwa na Bwana Compaore,ambae alikua naibu wake.

Mazingira ya kifo chake yamebakia kuwa si ya kufahamika.