Uhusiano wa Zika na ngono wachunguzwa US

Zika
Image caption Watafiti wa Marekani wamegundua visa 14 vya maambukizi ya Zika kupitia ngono

Maafisa wa afya nchini nchini Marekani wanachunguza taarifa nyingine 14 za uwezekano wa kuenezwa kwa virusi vya Zika kwa njia ya ngono. Visa hivyo vinahusisha wanawake kadhaa wawajawazito, kilieleza kituo cha CDC.

Kituo cha Marekani cha udhibiti wa magonjwa (CDC) kimefichua hayo wakati kikizindua muongozo mpya juu ya maambukizi ya virusi hivyo kwa njia ya ngono . Muongozo huo umetolewa kufuatia kuthibitishwa kwa kisa cha kwanza cha Zika kwa mtu ambae hakusafiri nchini Marekani.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption hakuna ushahidi kwamba wanawake wanawake wanaweza kuambukiza wapenzi wao Zika kwa ngono

Kisa hicho kilikuwa na uhusiano na tendo la kujamiiana na mpenzi alieambukia virusi vya Zika.

Kituo cha CDC kinawashauri wanaume wote ambao wamesafiri kwenye maeneo yenye virusi vya Zika kutumia mipira ya kondomu ama kuacha kufanya tendo la ngono kwa kipindi cha ujauzito.

Hakuna ushahidi bado kwamba wanawake wanaweza kueneza virusi vya Zika kwa wapenzi wao, lakini utafiti zaidi unahitajika kuelewa suala hili, kilieleza kituo hicho cha afya ya mwili.

Njia kuu ya maambukizi ya Zika kwa sasa bado ni kuumwa na mbu.

Haki miliki ya picha .
Image caption Hadi sasa njia kuu ya maambukizi ya Zika ni mbu

Wataalam wanasema wanawake wajawazito wanapaswa kujaribu kuepuka kuumwa na wadudu.

Jumanne, Margaret Chan, mkuu wa Shirika la Afya Duniani, alisema kuwa dunia inakabiliwa na "safari ndefu "ya kutokomeza Zika.

Akizungumza nchini Brazil, ambako visa vingi vimeripotiwa, alisema kuwa "virusi vya Zika ni vigumu, na itahitaji ujuzi wa hali ya juu " kuviangamiza.