Adele atawala tuzo za Brits

Image caption Adele

Adele ni malkia wa Uingereza,baada ya kushinda tuzo nne ikiwemo ile ya mwanamuziki bora pamoja na albamu bora.

''Kurudi baada ya mda mrefu na kupokewa kwa taadhima ni muhimu sana kwangu,''alisema.

Nyota huyo aliyefunga hafla hiyo kwa kucheza wimbo 'When we Were Young',pia alipokea tuzo ya wimbo bora nchini Uingereza pamoja na tuzo ya dunia ya ufanisi.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Adele ashinda tuzo 4 za Brits

Sherehe hiyo pia ilishirikisha kumbukumbu za marehemu David Bowie zilizoendeshwa na Annielennox na Gary Oldman.

Oldman baadaye alikubali tuzo kwa niaba ya mwanamuziki huyo na familia.