Zuma kuelekea Burundi kwa mazungumzo ya amani

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini anatarajiwa kuelekea nchini Burundi siku ya Alhamisi kwa mazungumzo yanayolenga kutatua mgogoro wa kisiasa nchini humo.

Bwana Zuma na viongozi wengine wa muungano wa Afrika wanaitaka serikali ya Burundi kuanzisha majadiliano na viongozi wa upinzani na kukubali kupelekwa kwa wanajeshi wa kulinda amani nchini humo.

Serikali tayari imesema kuwa haitazungumza na baaadhi ya maafisa wa upinzani ambao anaaamini hawako tayari kurudisha amani nchini humo.

Haki miliki ya picha
Image caption Rais Pierre Nkurunziza

Mgogoro huo ulianza baada ya rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu wa urais.

Ghasia zilizozuka zilifichua mgawanyiko wa kikabila uliokuwepo wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2000 uliowaacha watu 300,000 wakiwa wamefariki.