''Shekhe bandia'' akana kuipotosha mahakama UK

Image caption Shekhe Bandia

Mwanahabari mmoja mpekuzi aliyejulikana kama ''Shekhe Bandia'' amekana madai kwamba aliidanganya mahakama wakati wa kuvunjika kwa kesi ya ulanguzi wa mihadarati iliokuwa ikimkabili nyota wa muziki wa Pop Tulisa Constostavlos.

Mazher Mahmood mwenye umri wa miaka 52 kutoka eneo la Purley kusini mwa mji wa London,alikana kuipotosha mahakama katika kesi hiyo iliokuwa ikisikilizwa katika eneo la Old Bailey.

Mshtakiwa mwenza,Alan Smith mwenye umri wa miaka 66,dereva aliyestaafu kutoka Dereham,Norfolk pia alikana mashtaka hayo.

Wawili hao wameshtakiwa kwa kushirikiana kuipotosha mahakama kati ya Juni 22 na Julai 22, 2014.

Mashtaka yao yalisema kuwa Bwana Smith alibadilisha taarifa ilioandikwa na kuwapatia maafisa wa polisi wakati wa kesi ya jaji huyo wa zamani wa X factor.

Mwanahabari huyo mpekuzi ambaye alijifanya kuwa Shekhe wakati wa uchunguzi wake ,amedai kusaidia kuwakamata na kuwafunga zaidi ya wahalifu 100 wakati wa kipindi chake cha miaka 25 kazini.