Ripoti: BBC ilikosa fursa ya kudhibiti wadhalilishaji

Haki miliki ya picha PA
Image caption Jimmy Savile

Baadhi ya wafanyikazi wa BBC walifahamu mwenzao DJ Jimmy Savile, alikuwa akiwadhulumu wanawake na watoto lakini hakuweza kumshataki kwa wakuu wao kwa sababu ya hofu ambayo hata leo inaendelezwa katika shirika hili.

Ripoti huru iliyotayarishwa na bi Janet Smith imefichua.

Bi Smith alipewa jukumu la kufanya uchunguzi wa kina kwanini mtangazaji maarufu wa idhaa ya BBC aliweza kuwadhulumu kimapenzi wanawake 72 na hata kuwabaka wengine 8 bila ya wasimamizi wa idhaa hii ya BBC kugundua na kuchukua hatua kali dhidi yake.

Vilevile ripoti hiyo maalum imefichua kuwa mtangazaji mwengine bwana Stuart Hall aliwadhulumu kimapenzi wanawake 21 na hata wasimamizi wa BBC mjini Manchester walifahamu.

Mwenyekiti wa halmashauri ya BBC Rona Fairhead ameituhumu BBC kwa kushindwa kuwalinda wahasiriwa wa wawili hao.

''kwa kweli BBC iligeuka upande wa pili kana kwamba haikuona chechote kibaya hata pale ilipohiytajika kusimama wima na kutoa sauti dhidi ya visa hiyo,''

Kuhusu Savile na Hall, aliyehukumiwa kifungo mwaka wa 2013 baada ya kukiri kuwadhulumu kimapenzi wasichana 13 alisema ''Wale wote walioiamini BBC walitelekezwa wala hawakulindwa dhidi ya wawili hao''

Bi Janet amesema kuwa Savile, aliyeaga dunia mwaka wa 2011,na Hall walikuwa ni'' wapenda ngono'' na kuwa BBC ilikosa fursa mara tano ya kusitisha udhalilishaji huo wa watoto na wanawake .

Image caption Bi Janet amesema kuwa Savile, aliyeaga dunia mwaka wa 2011,na Hall walikuwa ni'' wapenda ngono''

Uchunguzi huo umebaini kuwa sifa ya Savile kama "mpenda ngono" ilikuwa inafahamika miongoni mwa baadhi ya wafanyakazi, lakini tuhuma hizo huenda hazikuwafikia viongozi.

Malalamiko rasmi yaliyotolewa mwaka 1977 na baba wa muathirika yalitakiwa kuripotiwa polisi, imesema ripoti hiyo.

Ripoti nyingine imesema "matendo ya habari ya Savile " yangeweza kutokea tena.

Ripoti ya Stoke Mandeville ilisema waathirika, walidhalilishwa kutoka mwaka 1968-92, na walikuwa na umri wa kuanzia miaka minane hadi 40.

Uchunguzi huu wa bi Smith uligharimu pauni milioni £6.5m kutoa ripoti hiyo yenye kurasa elfu moja 1,000 iliyogawanywa katika sura tatu.

Bi Smith alipewa jukumu la kufanya uchunguzi huru na BBC mwaka wa 2012 kuhusu sera za BBC ilipomuajiri Saville tangu mwaka wa 1964-2007.

Jaji huyo mstaafu aliwakashifu wawili hao kama watu waliotumia umaarufu wao kuwadhalilisha wanawake waliowatazama kama watu wenye hadhi ya juu katika jamii.