Mwanajeshi wa UN awaua wenzake

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi wa Chad wakifanya maombi

Mlinda amani wa taifa la Chad kaskazini mwa Mali amewauwa wanajshi wawili wa umoja wa Mataifa,kulingana na shirika la habari la AFP lililonukuu duru za umoja huo.

Anadaiwa kumuua kamanda wake pamoja na daktari.

Mauaji hayo yanafuatia hali ya wasiwasi kuhusu mazingira ya walinda amani hao,limeongeza AFP.

Makumi ya wanajeshi linda amani wa Chad hawafurahii mazingira yao ya kazi kaskazini mwa Mali.

''Mwanajeshi huyo aliamua kwamba hangekubali vile mkuu wake alivyokuwa akizungumza naye baada ya kushtumiwa kwa makosa makubwa,''kulingana na duru hizo.