Uchaguzi Iran: Kura zahesabiwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hassan Khamenei apiga kura Iran

Kura zinahesabiwa nchini Iran baada ya upigaji kura wa kuchagua bunge jipya na jopo la wataalamu ambalo humteua kiongozi mkuu wa nchi hiyo.

Muda wa kupiga kura uliongezwa mara kadha siku ya Ijumaa.

Uchaguzi huo ndio wa kwanza tangu Iran itie sahihi makubaliano na nchi zenye uwezo mkubwa duniani kuhusu mpango wake wa nuklia.

Waandishi wa habari wanasema kuwa hofu kubwa kwa wapiga kura wengi ni uchumi, ikiwa utainuliwa na makubaliano ya nuklia ambayo yalisababisha kuondolewa kwa vikwazo v