Wana mabadiliko waeleka kushinda Iran

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Uchaguzi Iran

Ripoti kutoka Iran zinasema kuwa matokea ya awali ya uchaguzi wa wabunge, yanaonesha kuwa wagombea wanaopendelea mabadiliko, wanaelekea kushinda kwa wingi mkubwa kabisa katika mwongo mzima.

Matokeo rasmi bado hayajatolewa, lakini ripoti zinasema, inaonyesha wagombea wasiopenda mabadiliko wamepoteza kura.

Ikiwa wabunge wanaopenda mabadiliko, na wanaotaka kuimarisha uhusiano na mataifa ya Magharibi, wakiongezeka, watampa nguvu Rais Hassan Rouhani.

Uchaguzi huo ndio wa kwanza, tangu Iran kutia saini makubaliano na mataifa makuu kuhusu mradi wake wa nuklia,mkataba uliopelekea karibu vikwazo vyote vya kiuchumi vya kimataifa dhidi ya Iran, kuondoshwa.