Zimbabwe kusherehekea miaka 92 ya Mugabe

Image caption Robert Mugabe

Maelfu ya watu wanatarajiwa kuhudhuria sherehe za kuzaliwa kwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ambaye alitimiza umri wa miaka 92 wiki iliyopita.

Wakosoaji wanasema kuwa sherehe hizo zinatarajiwa kugharimu takriban dola 800,000 wakisema kuwa ni fedha nyingi sababu ya hali ya ukame inayoikumba nchi hiyo.

Bwana Mugabe amekuwa madarakani tangu mwaka 1980 wakati Zimbabwe ilipowatimua wazungu kupata uhuru kamili kutoka nchini Uingereza.