KKK lawashambulia weusi kwa visu California

Image caption KKK lawashambulia weusi kwa visu California

Watu watatu wamedungwa visu katika mapigano kati ya kundi linalowachukia watu weusi la Ku Klux Klan (KKK) na waandamanaji wanaowapinga katika jimbo la California.

Tukio hilo lilitokea karibu na eneo kulikopangwa mkutano wa hadhara wa wazungu wao wanachama wa KKK.

Watu wanne walitiwa mbaroni katika makabiliano hayo, akiwemo mwanachama mmoja wa KKK aliyemdunga mweusi kisu.

Image caption Watu wanne walitiwa mbaroni katika makabiliano hayo

Msemaji wa polisi alieleza kuwa shida ilianza wakati wanachama wa KKK waliwasili katika uwanja wa Anaheim, karibu kilomita 50 Kusini Mashariki mwa Los Angeles, karibu na Disneyland.

Msemaji wa polisi alisema kuwa wanachama hao wa KKK walishambuliwa weusi walipokuwa wanatoka kwenye gari.

Mmoja aliangushwa chini.

Waandamanaji watatu wanaopinga KKK walidungwa visu katika makabiliano hayo.

Image caption Waandamanaji watatu wanaopinga KKK walidungwa visu katika makabiliano hayo.

Mtu mmoja aliyeshuhudia matukio hayo alisema kuwa wanachama wa KKK walikuwa wamelemewa.

Mmoja wa waliodungwa visu anaugua na amelazwa hospitalini.