Nigeria ina wafanyakazi hewa 24,000

Siku ya bajeti Nigeria Haki miliki ya picha Getty
Image caption Nigeria imelazimika kubana matumizi kutokana na matatizo ya fedha

Serikali ya Nigeria imeondoa karibu wafanyikazi 24,000 kutoka kwa orodha ya malipo ya wafanyikazi wa umma baada ya uchunguzi kugundua kwamba majina hayo yalikuwa ghushi. Wizara ya fedha imesema hatua hii imesaidia kuokoa kima cha dola bilioni 11.5.

Hii ni moja wapo ya kampeni ya kupambana na ufisadi aliyo ahidi Rais Muhammadu Buhari alipochukua mamlaka mwaka uliopita.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameahidi kupambana na ufisadi

Ufisadi na usimamizi mbaya wa fedha za umma zimetajwa kama vizingiti vikubwa dhidi ya ukuaji wa Nigeria, ambapo serikali imelazimika kubana matumizi kutokana na tisho la mdororo wa uchumi.

Nigeria ndiyo yenye uchumi mkubwa zaidi Barani Afrika na pia inaongoza katika uzalishaji wa mafuta imekumbwa na matatizo ya kifedha hususan kutokana na kuanguka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.

Nchi hiyo pia inakumbwa na mfumuko wa bei, kuanguka kwa soko la hisa huku uchumi huo ukiwa na ukuaji wa chini zaidi kuwahi kutokea kwa zaidi ya muongo mmoja.