Wageni wanaofanya makosa kufukuzwa Uswisi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wageni wanaofanya makosa kufukuzwa Uswisi

Dalili zinaonesha kuwa wapigaji kura watakataa pendekezo la kura ya maoni, kwamba wageni wanaofanya makosa madogo madogo ya jinai, wafukuzwe kutoka nchini Uswiswi.

Pendekezo hilo ni la chama cha mrengo wa kulia cha wananchi, SPP.

Chama hicho kinasema matatizo ya kijamii yanaambatana na idadi kubwa ya wageni.

Kufuatana na pendekezo hilo, mgeni yeyote anayerejelea makosa mawili madogo ya jinai katika miaka 10, atafukuzwa Uswiswi.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption SPP kinasema matatizo ya kijamii nchini Usiwsi yanaambatana na idadi kubwa ya wageni.

Vilevile wageni hao hawatokuwa na haki ya kukata rufaa.

Wanopinga pendekezo hilo, wanasema italenga robo ya watu wa nchi hiyo wanaotoka nje, na itaweka tabaka mbili katika sheria za nchi.