UN kuimarisha misaada Syria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Misaada ya kibinadamu Syria

Umoja wa Mataifa unapanga kutoa misaada ya kibinadamu kwa raia wa Syria laki moja unusu ambao wamekua kwenye maeneo ya vita, kufuatia muafaka wa kusitisha mashambulizi.

Umoja huo unasema unatarajiwa kuwafikia raia milioni 1.7 ifikapo mwisho wa mwezi Machi.Muafaka wa kusitisha mapigano uliafikiwa Jumamosi japo kumekua na madai ya maafikiano yao kukiukwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption MIsaada zaidi kuwasili huko Syria

Misaada ya kibinadamu ni pamoja na chakula, maji na dawa ambayo itapelekwa katika miji kama ule wa Madaya ambapo wakaazi wake wameripotiwa kufa njaa.Umoja wa Mataifa unakadiria kwamba karibu watu nusu milioni wamekwama katika maeneo ya vita nchini Syria.

Muafaka wa kusitisha mashambulizi ulifanikishwa kufuatia makubaliano kati ya Marekani na Urusi ambao wanaunga mkono makundi hasimu katika vita vya Syria. Hata hivyo mashambulizi dhidi ya makundi ya Islamic State na Nusra Front yanaendelea.