Watu milioni 3 hawana chakula Zimbabwe

Haki miliki ya picha AP
Image caption Watu milioni 3 hawana chakula Zimbabwe

Inakadiriwa kuwa watu milioni tatu nchini Zimbabwe wanakabiliwa na baa la njaa kufuatia ukame uliosababisha mifugo elfu 20,000 kufa.

Takriban wanyama 20,000 wamekufa, huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka maradufu.

Akiongea wakati wa sherehe za siku yake ya kuzaliwa, rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, alikiri kuwa taifa hilo linakabiliwa na madhara ya uhaba wa mvua kutokana na hali ya hewa ya El nino.

Zimbabwe inakabiliwa na hali kali zaidi ya kiangazi kuwai kushuhudiwa kwa kipindi cha miongo mitatu.

Kwa sasa, robo ya raia wa taifa hilo wanakabiliwa na uhaba wa chakula.

Maelfu ya wanyama pia wameangamia.

Rais Robert Mugabe tayari ametangaza hali hiyo kuwa janga la kitaifa, na hivyo inafungua njia kwa wafadhili kuingilia kati.

Tsvanginde Mutandavari anaishi katikia kijiji cha Tsvimborume , kilomota 400 kutoka Harare.

Anawategemea wanawe wawili wanaoishi Afrika Kusini kwa chakula, japo huwa nadra sana kwa wanawe kumtumia pesa.

Haki miliki ya picha
Image caption Zimbabwe inakabiliwa na hali kali zaidi ya kiangazi kuwai kushuhudiwa kwa kipindi cha miongo mitatu.

''hali inaendelea kudorora, ng'ombe wangu wanakufa. ikiwa hali hii haitabadilika, pia sisi tutaangamia . Nitalazimika kuuza ngombe wangu wote ili kuilisha familia yangu''.

''Mvua imenyesha siku za karibuni, afueni kwa wakulima wanaotarajia mavuno japo kwa uchache wake.''

Kwa kutangaza kiangazi kuwa janga la kitaifa, rais mugabe ambae ametawala Zimbabwe tangu mwaka wa 1980, anakwepa majukumu yake na serikali yake ya kuwalisha raia wa Zimbabwe.

Mugabe "umekuwa mwaka mbaya kwetu. Inabidi tutafute usaidize, tunahitaji pesa, pesa zaidi za kununua mahindi na aina nyingine ya nafaka. Nina uhakika kuwa tutafaulu kuondokana na tatizo linalotukabili."

Huku raia wa Zimbabwe wakilia njaa, sherehe ya kifahari ya kuadhimisha mika 92 kwa rais Mugabe iliandaliwa katika eneo la Masvingo, mojawapo wa maeneo yaliyoathiriwa sana na kiangazi.

Chama cha upinzani nchini humo Movement for Democratic Change kimeshikilia kuwa sherehe hiyo haikufaa, haswa wakati huu wa janga.