Mhubiri apatikana akivuta Cocaine UK

Image caption Mhubiri Crossan

Muhubiri mmoja wa kikatoliki aliyepatikana katika kanda ya video akivuta kile kilichojulikana kama dawa aina ya Cocaine amechukua likizo ya ukuhani.

Stephen Crossan ameripotiwa kuvuta Cocaine kwa kutumia noti ya pauni 10 katika usiku wa kunywa mnamo mwezi Julai 2015 katika eneo la Banbridge.

Alikuwa katika chumba kimoja chenye kumbukumbu za Nazi na alionekana akisema ''nisingefanya'' huku akivuta,Gazeti la the Sun jumapili liliripoti.

Askofu mkuu wa Dromore alisema katika taarifa kwamba hakuwa na ufahamu kuhusu kisa hicho.

Kisa hicho kinadaiwa kutokea katika chumba cha parokia mwezi Julai baada sherehe.

Gazeti la The sun jumapili limedai kuwa kilitendeka katika ile iliojulikana kama nyumba ya parokia ya Crossan katika kanisa la St Patrick Banbridge mwaka 2015.

Image caption tai

Crossan aliliambia gazeti hilo kwamba alitumia dawa hiyo lakini akasema:''Ilikuwa usiku mmoja pekee''.

Duru moja ilisema kwamba kundi moja lilikuwa na mhubiri huyo baada ya sherehe na lilipata kumbukumbu za Nazi ikiwemo bendera,kofia na tai.

Akijitetea Crossan aliliambia gazeti hilo kwamba yeye si Nazi na kwamba alikusanya vifaa vya kihistoria kutoka kila taifa.