Jaji Thomas wa Marekani avunja ukimya

Jaji Clarence Thomas wa mahakama kuu nchni Marekani amevunja ukimya wa miaka 10 wa kutouliza swali mahakani wakati wakichangia hoja siku ya Jumatatu.

Jaji Thomas alivunja ukimya huo wakati wa kusikiliza kesi inayohusu haki ya kumiliki silaha, alipomuuliza maswali 10, wakili kutoka Wizara ya sheria ya Marekani, ambaye alikuwa akiitetea sheria ya nchi inayopiga marufuku mtu mwenye kosa dogo la unyanyasaji wa kijinsia, kuzuiwa kumiliki silaha.

Chini ya sheria za nchi mtu yoyote anayetiwa hatiani na makosa ya jinai, anaondolewa katika vigezo vya kumiliki silaha.

Zuia hilo pia linamhusu yoyote mwenye hatia ya unyanyasaji.

Kwa mara ya mwisho Jaji Thomas aliripotiwa kuuliza swali Februari 2006, katika mahakama kuu wakati wa kesi iliyotolewa adhabu ya kifo.

Amezungumzia hilo wiki kadhaa baada ya kifo cha mmoja wa wanachama wa mahakama kuu Jaji Antonin Scalia,

Mahakama nchini humo inafikiria kuweka mipaka mipya kuweza kufikia sheria ya nchi kupigia marufuku watu waliotiwa hatiani na unyanyasaji wa kijinsia kuweza kumiliki silaha.