Kylie Minogue na Kylie Jenner wapigania jina

Haki miliki ya picha 20th century fox
Image caption Kylie Minogue

Mwanamuziki nyota Kylie Minogue anajaribu kumzuia ''Kylie'' Jenner kutotumia jina Kylie kama nembo yake nchini Marekani.

Na mawakili wa mwanamuziki huyo hawataki vita.

Wamewasilisha stakhabadhi mahakamani wakisema kwamba nyota huyo wa kipindi cha ''keeping up with the Kardashians'' hana umuhimu mkubwa katika kipindi hicho na kwamba huonekana katika ''maonyesho ya picha''.

Wamesema kuwa kumpatia nembo ya Kylie J kutamuharibia Minogue nembo yake ya Kylie M.

Image caption Kylie Jenner

Stakhabadhi hizo zinamuelezea Kylie Jenner kama ''msichana aliyehitimu masomo nyumbani'' zikisema kwamba onyesho lake la picha na machapisho yake yamezua hisia kali kutolka kwa makundi ya watu walio na ulemavu pamoja na jamii za Waafirika wa Marekani.

Hilo lilionekana wakati Kylie Jenner alipopiga picha akiwa katika baiskeli ya walemavu mbali na hisia alizopata baada ya kuchapisha picha za nywele zake katika mtandao wa instgram.

Mashabiki wa mwanamuziki huyo pia wanamuunga mkono wakisema kuwa katika tweeter kwamba #TheresOnlyOneKylie.

Wengine wanasema kuwa kuna Kylie M mmoja kwa kuwa hawamjui Jenner ni nani.