Pakistan kumzika aliyemuua Gavana

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mlinzi wa zamanni wa Gavana wa Punjab, Qadri Mumtaz

Pakistan inajiandaa kushuhudia maandamano zaidi wakati wa mazishi ya mlinzi wa zamani aliyemuua Gavana wa jimbo la Punjab, tukio lililoshtua wengi nchini humo.

Mamlaka zimepeleka vikosi vya usalama katika eneo la Rawalpindi ambapo maelfu ya Watu wanatarajiwa kuomboleza kifo cha Mumtaz Qadri.

Qadri alisifiwa na wanamgambo wa kiislamu kuwa shujaa baada ya kumuua Salman Taseer mwaka 2011.

Kifo chake siku ya jumatatu kilisababisha maelfu ya waandamanaji kuingia mtaani nchini Pakistan.

Watu wanaomuunga mkono Qadri walifanya maandamano ya amani mjini Karachi,Lahore,Islamabad na kufunga njia za kuingia Islamabad.

Waandamanaji walichoma magurudumu na kuimba nyimbo.

Qadri aliwafunza polisi makomandoo na kupewa jukumu la kumlinda Salman Taseer,Qadri alimpiga risasi mwanasiasa katika soko moja mjini Islamabad mwezi januari mwaka 2011, na baadae mwaka huo alihukumiwa kifo.

Alisema aliwajibika kwa dini yake kumuua Waziri,ambaye alikuwa akipinga Sheria za Pakistan alizoamini kuwa kandamizi.