Kaburi la Shakespeare kuchunguzwa

Image caption Shakespear

Utafiti wa kutumia rada ndani ya kaburi la William Shakespeare na uchimbaji wa nyumba ya mwandishi huyo maarufu ni miongoni mwa miradi ya miaka 400 ya maadhimisho ya kifo chake.

Kaburi la Shakespeare katika kanisa la Holy Trinity huko Straford halijachimbuliwa lakini uchunguzi unafanywa ili kutafuta kilicho ndani yake.

Hatua hiyo inaruhusu uchunguzi bila ya kuliharibu kaburi lenyewe.

Matokeo yake yanatarajiwa kutolewa katika majuma kadhaa yajayo.

Inaaminika kuna ugunduzi katika kaburi hilo lililopo ndani ya kanisa ambalo familia ya Shakespear ilizikwa.

Kumekuwa na uvumi kwamba kuna chumba kilichotengewa familia hiyo chini ya mawe na kuna maswali mengi kuhusu iwapo uchunguzi huo utaonyosha vitu vilivyozikwa na mtunzi huyo wa vitabu.

Kaburi ambalo Shakespear amezikwa mwaka 1616 limeandikwa onyo hili:

''Marafiki wa Yesu musichimbe udongo huu,atakayebarikiwa awe mtu ambaye atahifadhi mawe haya na atakayelaaniwa ni yule ambaye atahamisha mifupa yangu''.