Mashambulizi mapya Syria kuchunguzwa

Image caption Usitishwaji wa mapigano umefanikisha shughuli za binadamu

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesema madai yote ya kuvunja muafaka wa kusitisha mashambulizi nchini Syria yatachunguzwa.

Hata hivyo Kerry amesisitiza kwamba Marekani na Urusi wameafikiana kutojadili madai hayo hadharani.

Image caption Watoto wameanza kucheza baada ya mashambulio kusimama

Ameongeza pande hizo zimekubaliana kuhakikisha mashambulizi yanalenga ngome za wapiganaji wa Islamic State na Al-Nusra Front pekee.

Makundi hayo hayajawekwa kwenye muafaka wa kusitisha mapigani kwa muda ili kuwezesha shughuli ya kusambaza misaada ya kibinadamu nchini Syria.