Maswala 5 kuu kuhusu kambi ya Calais

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Maafisa wa utawala katika bandari ya Ufaransa ya Calais wanaendelea kubomoa na kuondoa makaazi ya muda

Maafisa wa utawala katika bandari ya Ufaransa ya Calais wanaendelea kubomoa na kuondoa makaazi ya muda ya wahamiaji yajulikanayo kwa jina Jungle.

Mamlaka ya Ufaransa imesema wanataka kuwaondoa wahamiaji 2,000 wanaoishi katika eneo hilo.

Wahamiaji ni nani?

Inakadiriwa kuwa idadi ya wakazi kwenye kambi hiyo ijulikanayo kama 'Jungle' inatofautiana.

Maafisa wa Calais wanasema wanatunza wakazi 3,700, huku taasisi ya msaada kwa wakimbizi ikisema kambi hiyo ina watu takriban 5,500.

Wahamiaji wengi katika kambihiyo ni wakimbizi kutoka nchi zinazokumbwa na mapigano kama Syria,Afghanistan Iraq na wengine wanakimbia ukiukwaji wa haki za binaadam nchini Eritrea.

Lakini wengine wanatoka nchi za kiafrika ambazo hazina ripoti ya kuwepo kwa migogoro hivi karibuni.

Kumekuwa na ukosoaji kuwa hawa ni wahamiaji wa kiuchumi wanaosaka maisha mazuri ughaibuni.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Kuna wanawake 205 na Watoto 651(423

Kuna wanawake 205 na Watoto 651(423, kati yao hawana watu wazima waliofika nao) katika kambi, taasisi ya Help Refugees imeeleza.

Kwa nini wako Calais?

Kambi iko Calais nchini kwenye mpaka wa Ufaransa kwa sababu wahamiaji wanajaribu kuingia Uingereza, na Calais ni sehemu panapoanzia njia ya reli na pia bandari.

Wahamiaji wengi wanajaribu kuingia Uingereza kwa kujificha kwa kuingia kwenye magari ya kubeba mizigo, treni na hata kupanda vivuko vinavyokwenda Uingereza.

Mwaka 1999, Kambi ya wakimbizi ya Sangatte ilifunguliwa mjini Calais, ikivutua maelfu ya watu wanaotafuta hifadhi na watu waliouzwa.

Kufungwa kwake mwaka 2002 kwa amri ya waziri wa wakati huo wa mambo ya ndani Nicolas Sarkozy kulisababisha vurugu.

Tangu wakati huo wahamiaji wameendelea kuwasili Calais na kujenga makazi ya muda mfupi karibu na bandari.

Kwa nini wanataka kwenda Uingereza?
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wahamiaji wanaishi Calais kwa muda kwa azimio kuwa siku moja wataweza kuingia Uingereza

Wengi wanataka kupata hifadhi Uingereza.

Wengine wanataka kuingia nchini humo bila kutambulika na kuendelea kubaki kuwa wafanyakazi wasio na vibali.

Natacha Bouchart, Meya wa Calais amesema wahamiaji haramu wanaiona Uingereza kuwa ni rahisi kujipatia faida na ni rahisi kupata kazi kuliko Ufaransa, hata hivyo hilo haijathibitishwa.

Pia ameeleza sababu nyingine ni kuwa Wahamiaji wanakwenda huko kwa kuwa hakuna mfumo wa kitaifa wa vitambulisho na polisi hawawezi kuwasimamisha watu mitaani kuonyesha vitambulisho.

Shirika la msalaba mwekundu nchini Uingereza limesema wahamiaji wanataka kuingia Uingereza kwa kuwa wanaamini kuna mafanikio katika kutafuta kazi au kwa kuwa wanajua kuzungumza Kiingereza na wanataka kukitumia.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Calais ni mji wa bandari ulioko kwenye mpaka wa Ufaransa na Uingereza

Wengine wana ndugu huko lakini pia wanaamini kuwa kuna makaazi mazuri na elimu nzuri .

Kwa nini wanafunga Kambi?

Mamlaka ya Ufaransa inataka kuwahamisha wakazi katika eneo jipya lililojengwa kwa kontena zilizotumika na kuzingirwa kwa nyaya na kupewa ulinzi saa 24.

Operesheni hiyo imeanzia kusini mwa nchi hiyo,ambapo mamlaka inaamini watu takriban 1000 wanaishi huko.

Mashirika ya misaada yanasema kuwa idadi hii imepewa makisio ya chini kwa kuwa idadi ni kubwa mara tatu yake.

Mhamiaji mmoja ameiambia BBC kuwa ni bora kuishi mtaani.

Image caption Natacha Bouchart, Meya wa Calais amesema wahamiaji haramu wanaiona Uingereza kuwa ni rahisi kujipatia faida na ni rahisi kupata kazi kuliko Ufaransa

Wengine wameona ni bora kupelekwa kwenye kambi nyingine ambayo itawawezesha kufika Uingereza.

Wahamiaji hawa wanahofu kuwa watalazimika kutuma maombi ya kupata hifadhi Ufaransa kuliko Uingereza ikiwa wataishi kwenye makontena.

Ripota wa BBC anasema kuna nafasi chini ya 300 zilizo wazi katika makotena kwa ajili ya wakazi takriban 3,000 kambini humo.