EU kuanzisha msaada wa dharura wa wahamiaji

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wahamiaji

Muungano wa Ulaya unajiandaa kutumia mamilioni ya dola kwa ajili ya misaada ya kibinadamu katika kipindi cha miaka mitatu ijayo, kuisaidia Ugiriki kukabiliana na maelfu ya maelfu ya wakimbizi na wahamiaji walioingia nchini humo .

Kwa mujibu wa mipango itakayoidhinishwa na tume ya Muungano wa Ulaya baadae leo, pesa hizo zitatolewa na Ulaya kama zinavyotolewa kwa ajili ya kumaliza mizozo kwenye maeneo mengine ya dunia.

Ikiwa utakubalika mashirika ya misaada ya EU kwa mara ya kwanza yatafanya kazi moja kwa moja na Umoja wa mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali ndani ya Muungano wa Ulaya , badala ya kupata pesa kutoka kwa nchi moja kama vile Ugiriki.

Maafisa wa muungano huo wanasema kuwa mpango huo utatenga Yuro milioni 300 mwaka huu ili kulisaidia taifa lolkote la muungano huo kukabiliana na tatizo la wahamiaji.

Fedha hizo zipatazo yuro milioni 700 zitatumika kwa kpindi cha miaka mitatu.

Hatahivyo mwandishi wa BBC barani Ulaya Chris Morris amesema kuwa iwapo fedha hizo zitawasilishwa kwa haraka ,muungano huo pia utakabiliana na wahamiaji wapya.

Hatua hiyo itaamanisha ushirikiano mzuri na Uturuki.