Njia za ajabu za kutafuta bahati katika mtihani Asia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanafunzi hutumia mbinu tofuati kupasi mitihani yao
Wakati wa mtihani huwa mgumu kwa watu wengi, hususan Asia mashariki ambapo kuna shinikizo kubwa kwa watu kufaulu.

Licha ya tofuati za kitamaduni, wanafunzi wote wana itikadi na imani zao, iwe ni kuimba nyimbo, kula chakula maalum au hata kuvaa nguo wanaoiona kuwa na bahati kwao.

Hizi ni baadhi ya mbinu zinazotumika kote Asia na wanafunzi kuhakikisha wanafualu kwa ukubwa:

1. Kula tufaha kila siku

Image caption Tunda la kusoma: tufaha huliwa kwa wingi

Migahawa katika vyuo vikuu Hong Kong huwapa wanafunzi matufaha na vyakula vinavyotengenezwa kutokana na tufaha wakati mitihani ikikaribia.

"Tufaha katika Kichina hutamkwa "ping guo", yaani "salama". Kwa hivyo inadhaniwa utapasi mtihani salama," anasema Chong Wang, kutoka Nanjing China.

2. Epuka kuosha nywele

Haki miliki ya picha THINKSTOCK
Image caption Ukiosha nyele, unaosha elimu kichwani

Iwapo umsahau kuoga na zaidi kuosha nyele katika harakati zako za kila siku, usiwe na wasiwasi, huko Korea kusini inadhaniwa kuwa mtu akiosha nywele zake anaosha elimu yote kichwani.

"Kulikuwa na kijana mmoja ambaye alikuwa haoshi nywele zake kabla ya mtihani, alikuwa msafi wakati mwingine wote ila siku ya mtihani huwezi kumkaribia," amesema mwanamfunzi mmoja kuhusu mwenziwe darasani.

3. Kula korosho

Haki miliki ya picha THINKSTOCK
Image caption Neno 'korosho' lina maana 'hamu ya kupita' Kichina

Mwezi mmoja kabla ya mitihani Hong Kong, wanafunzi hukusanyika kwa shughuli mbalimbali zinazoanza kwa chakula cha jioni kijulikanacho kama ging guo.

Inaaminika shughuli hizo husaidia wanafunzi kupita mitihani kwa alama za juu.

Ni muhimu kwa wanafunzi katika dhifa hizo kula nyama ya nguruwe na korosho.

Na chakula hicho hupatikana katika migahawa ya Kichina ambapo korosho kwa Kichina ni neno sawa na neno "kutarajia kupasi", na "nyama ya nguruwe" ni sawa na "hamu ya kupata alama ya juu".

4. Nguvu ya kuku

Image caption Supu ya kuku ina faida ipi kwa akili?

Supu ya kuku inadhaniwa kuchangamsha ubongo.

Wanafunzi wa Malaysia, Hong Kong, Singapore na China hunywa supu ya kuku wanaposoma kujitayarisha kwa mitihani na asubuhi ya kuamkia mtihani wenyewe.

"Sio uchawi," anasema Dylan Lee Soon Yoong, mwanafunzi kutoka Singapore katika chuo kikuu cha London.

"Nilikunywa supu ya kuku asubuhi kuamkia mtihani ikiwa moto moto. Inatakikana kukusaidia kuwa makini zaidi na wanafunzi huinywa kwa wingi Singapore."

5. Vaa chupi nyekundu

Haki miliki ya picha THINKSTOCK
Image caption Nyekundu ina bahati yake

Rangi nyekundu inaaminika kwa kwa kiwango kikubwa nchini China kuwa ni rangi ya bahati.

Kwa hivyo watu wengi wanaamini ni vizuri kuvaa nguo nyekundu na zaidi nguo za ndani za rangi nyekundi wakati wa mtihani.

Wakati mtu anapofanikiwa kuna msemo wa Kichina unaosema, "umevaa nguo ya ndani nyekundu?"

Lakini Chong Wang anaonya kwamba si wote wanaoiamini rangi hiyo.

"Baadhi ya watu huepuka kuvaa rangi nyekundu wakati wa mtihani kwa sababu nchini China alama za kufeli huandikwa kwa rangi nyekundu," anasema.