8 wauwa katika mapigano Jordan

Image caption Operesheni inaidaiwa kuwalenga wafuasi wa IS

Maafisa wengine wanne pia wamejeruhiwa katika mapigano yaliozuka kufuatia uvamizi unaorifiwa kuwalenga wapiganaji jihadi ulioanza Jumanne usiku na kumalizika muda mfupi kabla ya lafjiri siku ya pili.

Duru ya usalama inaarifu waliolengwa ni wafuasi wa Islamic State (IS)

Jordan ni mwanachama wa muungano unaooongozwa na Marekani dhidi ya kundi lililopo katika nchi jirani za Syria na Iraq.

Ufalme huo umetekeleza mashambulio ya anga katika maeneo yanayodhibitiwa na IS huko Syria mnamo September 2014, kuhakikisha utulivu na usalama wa mipaka yake.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Washukiwa 30 pia walikamatwa

Operesheni hiyo huko Irbid inadaiwa kuwa kubwa dhidi ya kinachoshukiwa kuwa mtandao wa wapiganaji jihadi katika kipindi cha miaka mingi.

Msemaji wa serikali Mohammad Momani amekiambia kituo cha redio cha usalama wa umma amewataja walengwa kama wahalifu wakuu lakini hakutoa ufafanuzi zaidi.

Duru ya usalama imeliambia shirika la habari la Reuters kuwa wahalifu hao ni wafuasi wa IS na kwamba walizingirwa katika nyumba ya makaazi karibu na kambi ya wakimbizi wa Palestina katikati mwa Irbid.

Kiasi ya washukiwa 30 pia walikamatwa katika operesheni hiyo, duru hiyo iliongeza.