Korea Kaskazini kususia mikutano ya UN

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Korea Kaskazini

Korea Kaskazini imesema kuwa itasusia kushiriki katika mkutano wa baraza la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za kibinaadamu ambalo linachunguza rekodi yake.

Waziri wa maswala ya kigeni Ri Su yong amelishtumu baraza hilo kwa kuweka siasa,ubaguzi na upendeleo na kuilenga Korea Kaskazini mara kwa mara.

Baraza la Umoja wa Mataifa limekosoa Korea kaskazini kwa vile inavyowanyanyasa raia wake.

Hatua hiyo huenda ikazidi kuitenga Korea Kaskazini ambayo inakabiliwa na vikwazo vipya.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa linatarajiwa kupiga kura siku ya Jumatano kuhusu vikwazo hivyo ,ili kujibu hatua ya Korea Kaskazini kuzifanyia majaribio zana za kinuklia mbali na uzinduzi wake wa Satelite.

Hatua zote mbili zinakiuka vikwazo vilivyopo.

Katika taarifa yake kwa baraza hilo,bwana Ri pia ameishtumu Marekani na mataifa mengine kwa ushahidi wao.

Amesema kuwa Korea kaskazini haitatimiza mahitaji yoyote yatakayoafikiwa na baraza hilo.