Wauawa kwa kumiliki mifupa ya albino

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Albino huuawa Malawi kwa itikadi za kichawi
Polisi wanasema umati wa watu uliwamwagiya watu hao petroli na kuwawasha moto katika kijiji kilichopo kusini mwa nchi hiyo.

Mifupa hiyo inaaminika kuwa ya watu wenye ulemavu wa ngozi - albino.

Sehemu za mwili zinadhaniwa kuleta bahati na mara nyingi hutumika kwa uchawi.

Umoja wa mataifa unasema walemavu takriban tisa wameuawa Malawi katika mwaka uliopita.

Sehemu za mwili za Albino hutumiwa pia katika nchi jirani ya Tanzania na Msumbiji.