Kiranja wa ANC bungeni ajiuzulu

Haki miliki ya picha
Image caption Kiranja wa chama tawala cha ANC bungeni amejiuzulu wadhfa wake.

Kiranja wa chama tawala cha ANC bungeni amejiuzulu wadhfa wake.

Bwana Stone Sizani alijiuzulu wadhfa wake bungeni na pia katika chama cha African National Congress (ANC).

Hatua hiyo ya bwana Sizani imewadia wakati ambao rais Jacob Zuma anakabiliwa na shinikizo kubwa la kumtaka awajike na kujiuzulu kwa ubadhirifu wa mali ya umma.

Aidha Zuma anashinikizwa na wabunge wa upinzani waliokwenda mahakamani kumtaka ang'atuke madarakani kwa kutumia vibaya mamlaka yake na kukosa uadilifu alipokosa kulipia gharama ya ukarabati wa nyumba yake.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bwana Stone Sizani alijiuzulu wadhfa wake bungeni na pia katika chama cha African National Congress (ANC).

Hapo jana Zuma alinusurika kura ya kutokuwa na imani naye bungeni kutokana na wingi wa wabunge wa chama cha African National Congress (ANC) bungeni.

Rais Zuma amekanusha madai kuwa ameihujumu uchumi wa Afrika Kusini na kupalilia ubadhirifu wa mali ya umma kupitia kwa rushwa na ufisadi.

Sizani hajaelezea kwanini amejiuzulu wadhfa wake huo.

Hata hivyo raia wa Afrika Kusini wamekuwa wakishuku kauli yake inatokana na kukithiri kwa ufisadi serikalini.