Sudan Kusini yajiunga na Afrika Mashariki

Haki miliki ya picha AFP
Image caption South Sudan yajiunga na EAC

Taifa changa zaidi duniani, Sudan Kusini , limejiunga na jumuiya ya mataifa ya Afrika Mashariki.

Sudan Kusini imejiunga rasmi na muungano huo katika hafla ya kongamano la viongozi wa mataifa wanachama wa EAC unaoendelea mjini Arusha Tanzania.

Viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki walikutana katika kikao cha 17 cha marais.

Kujiunga kwa Sudan Kusini kumefikisha idadi ya mataifa wanachama kufikia 6.

Mataifa mengine wanachama ni Kenya, Burundi, Rwanda, Tanzania na Uganda.

Haki miliki ya picha Statehouse Tanzania
Image caption Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli alitawazwa mwenyekiti mpya wa muungano huo.

Katika kongamano hilo la viongozi, rais mpya wa Tanzania John Pombe Magufuli alitawazwa mwenyekiti mpya wa muungano huo.

Rais Magufuli atahudumu katika wadhfa huo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Viongozi wa mataifa wanachama vilevile walishuhudia kuapishwa kwa Liberat Mfumukeko kuwa katibu mkuu wa muungano huo .

Rais huyo wa Burundi anachukua pahala palipoachwa wazi na kustaafu kwa katibu wa zamani Richard Sezibera ambaye muda wake ulikamilika.