Trump na Clinton watawala Jumanne Kuu

Clinton Haki miliki ya picha Reuters AFP
Image caption Bw Trump na Bi Clinton wote wawili wameshinda majimbo saba kufikia sasa

Mgombea wa Democratic Hillary Clinton na mgombea wa Republican Donald Trump wameshinda majimbo mengi katika mchujo wa kuteua wagombea urais Marekani katika vyama vyao Jumanne Kuu.

Wagombea wote wawili wameshinda majimbo saba kila mmoja. Wameshinda wote wawili majimbo ya Alabama, Georgia, Tennessee na Virginia.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Clinton ameshinda majimbo matano

Bi Clinton pia ameshinda Arkansas na Texas, naye Bw Trump akashinda Massachusetts.

Bw Trump hata hivyo ameshindwa na Seneta Ted Cruz majimbo ya Texas, Alaska na Oklahoma.

Mgombea wa Democratic Bernie Sanders naye ameshinda kwake nyumbani katika jimbo la Vermont, Minnesota, Colorado na pia katika jimbo la Oklahoma.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Donald Trump anaongoza chama cha Republican

Mchujo wa Jumanne Kuu hushuhudia majimbo 11 yakifanya mchujo kwa pamoja huku maandalizi ya uchaguzi mkuu tarehe 8 Novemba yakiendelea kushika kasi.

Bi Hillary Clinton, aliyekuwa wakati mmoja waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, pamoja na mfanyabiashara tajiri kutoka New York Donald Trump walipigiwa upatu kushinda majimbo mengi Jumanne Kuu.

Utafiti wa maoni ya baada ya kura ulikuwa umeonyesha Trump na gavana wa Ohio John Kasich wakikabiliana vikali katika mchujo wa chama cha Republican jimbo la Vermont, lakini baadaye Trump aliibuka mshindi.

Bi Clinton na Bw Sanders pia walikabiliana vikali katika jimbo la Massachusetts, kaskazini mashariki mwa Marekani lakini Clinton akaibuka mbabe.

Matokeo kwa sasa:

Donald Trump (Republican): Alabama, Georgia, Massachusetts, Tennessee, Virginia, Arkansas, Vermont

Ted Cruz (Republican): Texas, Oklahoma, Alaska

• Marco Rubio (Republican): Minnesota

Hillary Clinton (Democratic): Alabama, Georgia, Tennessee, Virginia, Arkansas, Texas, Massachusetts

Bernie Sanders (Democratic):Vermont, Oklahoma, Minnesota, Colorado