Kampuni kuwapatia likizo walio katika hedhi

Image caption Mkurugenzi wa kampuni ya Co-Exist Bex Baxter

Kampuni moja ina mpango wa kuwaruhusu wanawake kuchukua likizo wakati wanapoingia katika hedhi.

Kampuni hiyo kwa jina Co-Exist iliopo mjini Briston nchini Uingereza inasema kuwa wanawake wataruhusiwa kupumzika nyumbani wakati wanapokuwa na hedhi na baadaye kuhudumia wakati huo kazini.

Mkurugenzi Bex Baxter ameliambia gazeti la Bristol Post kwamba wanawake uhisi uchungu wakati wa hedhi lakini hawataki kwenda nyumbani.

Likizo za hedhi hutolewa nchini Japan ,maeneo kadhaa ya Uchina Korea Kusini na Taiwan.

Inadaiwa kuwa kampuni hiyo ni ya kwanza kuzindua mpango huo barani Ulaya.

Kampuni hiyo imewaajiri watu 24, saba wakiwa wanaume.

Bi Baxter amesema kuwa maelezo ya sera hiyo hayajafanyiwa kazi lakini yatazungumzwa katika mkutano baadaye mwezi huu.