Watuhumiwa kulilipua shamba la maziwa

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES
Image caption Shamba hilo la maziwa ni la jamaa ya rais Mugabe
Gazeti la serikali - Herald - linaariifu kuwa waendesha mashtaka wamewarudishia mashtaka wanajeshi wawili wanaotuhumiwa kulilipuwa kwa bomu la petroli shamba la maziwa linalomilikiwa na familia ya rais Robert Mugabe.

Linaarifu kwamba, hatua hiyo inakiuka uamuzi wa mwendesha mashtaka mkuu kutupilia mbali mashtaka hayo dhidi ya wanajeshi hao wenye umri wa miaka ya 29 na 37.

Mawakili wa wanajeshi hao wanashinikiza kesi itupiliwe mbali wakieleza kuwa haiwezekani kwa Tomana kugeuza kauli yake na kuamuru washtakiwe.

Herald imeripoti, mawakili wa serikali wanasema naibu wa Tomana alichukua uamuzi huo wa kuwashtaki upya wanajeshi hao baada ya kufuata sheria zinazazohitajika.

Tomana ameachiliwa kwa dhaman baada ya uamuzii wake kumsababisha kushtakiwa kwa kuzuia sheria itendeke.

Amekana mashtaka.