Mitt Romney asema Trump ni 'tapeli'

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mitt Romney

Aliyekuwa mgombea wa urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani Mitt Romney amekitaka chama chake kumkataa Donald Trump ,akimtaja mgombea huyo aliye kifua mbele kuwa ''tapeli''.

Bwana Romney amemshtumu Bwana Trump kwa kuwachukulia raia wa Marekani kama wajinga katika hotuba ya siri iliotolewa kwa vyombo vya habari.

Bwana Trump hatahivyo amemkejeli bwana Romney katika mtandao wa tweeter kama mgombea aliyefeli na ambaye hafai kutoa ushari wowote kuhusu uchaguzi.

Viongozi wakuu wa chama cha Reupblican wameshangazwa na vile bwana Trump anavyoelekea kushinda tiketi ya chama cha Republican kwa uchaguzi huo wa mwezi Novemba.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Donald Trump na Hillary Clinton

Inadaiwa kuwa wanachama kadhaa wa kamati ya kitaifa kuhsu usalama wa jamii waliandika barua ya wazi wakielezea maono ya bwana Trump kama yasio na msingi wala sera.

Bwana Trump amejiwasilisha kama muunganishi kufuatia ushindi wake katika majimbo saba katika ile ilipotajwa kuwa jumanne maalum na hivyobasi kuimarisha uongozi wake katika chama chake.

Romney ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa Trump anatarajiwa kutoa onyo katika hotuba yake siku ya Alhamisi,kwamba sera za bwana Trump ni tishio kwa chama cha Republican na taifa zaima kwa jumla.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Donald Trump

Bwana Romney pia ataonya kuwa uteuzi wa Trump utarahisisha harakati za Bi Hillary Clinton kushinda urais nchini humo.