Utafiti:Nyakati za raha zinaweza kukuharibu moyo

Image caption Ugonjwa wa Takatsobu

Msongo wa mawazo ambao husababisha maumivu katika kifua na mtu kushindwa kupumua hutokea wakati wa raha na hasira ,huzuni na hofu,utafiti nchini Uswizi umebaini.

Robo tatu ya visa vya ugonjwa wa Takotsubo ambao hubadili umbo la moyo na kusababisha kifo hutokana na msongo wa mawazo.

Utafiti huo uliofanywa katika hospitali ya Zurich na kuchapishwa katika jarida la moyo barani Ulaya,unasema kuwa kila kisa kimoja kati ya 20 husababishwa na raha.

Tatizo hilo huwa ni la mda na watu hurejelea hali yao ya kawaida baadaye.

Katika utafiti huo wa wagonjwa 1750,watafiti walibaini matatizo ya moyo yanayosababishwa na:

  • Sherehe ya kuzaliwa
  • Harusi ya mtoto wa kiume
  • Kukutana na rafiki baada ya miaka 50
  • Kufikia umri wa kuitwa bibi.
  • Timu unayoipenda kushinda mechi.
  • Kushinda bahati nasibu.

Utafiti huo pia umesema kuwa visa vingi huwatokea wanawake waliomaliza kuzaa.

Daktari Jelena Ghadri,mmoja ya watafiti anasema:Tumebaini kwamba ugonjwa huo unaweza kusababishwa na sababu mbali mbali na ilivyotarajiwa.

Mtu mwenye ugonjwa huo wa Takotsubo sio aliyevunjika moyo kwa sababu baadaye mtu huyo anaweza kuwa mwenye furaha.