Vikosi vya Libya vyashambulia maficho ya IS

Image caption libya_Islamic State

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Libya amesema kuwa mateka wawili raia wa Italy waliotekwa nyara mnamo mwezi Julai huenda wameuawa nchini Libya kufuatia uvamizi wa vikosi vya Libya katika maficho yaliotumiwa na wapiganaji wa Islamic State.

Nyumba moja ya shambani kusini magharibi mwa mji wa Sabratha ilivamiwa kufuatia taarifa iliotolewa na wapiganaji wa Islamic State waliokamatwa wiki iliopita.

Meya wa Sabratha ameiambia BBC kwamba anaamini kwamba 2 kati ya 12 waliouawa katika shambulio hilo walikuwa wajenzi hao raia wa Itali.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Libya

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Itali amesema kuwa bado anajaribu kuhakiki ripoti mbali na kuchunguza picha za waliouawa.

Raia 4 wa Itali kutoka kwa kampuni inayotoa huduma za mafuta na gesi Bonatti walitekwa nyara na watu wasiojulikana mnamo mwezi Julai,karibu na mpaka wa Libya na Tunisia.