Malaysia:Mabaki ni sawa na yale ya MH370

Haki miliki ya picha Blaine Alan Gibson
Image caption Mabaki yaliopatikana katika mchanga wa baharini nchini Mozambique

Waziri wa uchukuzi nchini Malaysia amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba mabaki yaliopatikana nchini Mozambique ya ndege aina ya Boeng 777 ni sawa na yale ya ndege ya Malaysia iliopotea ya MH370.

Australia imesema kuwa eneo hilo ni miongoni mwa maeneo ambapo mawimbi baharini huyasukuma mabaki.

Image caption Bawa la ndege ya MH£&) lilipatikana katika kisiwa cha Ufaransa cha Reunion

Bamba hilo lenye urefu wa mita moja lilipatikana katika mchanga wikendi iliopita.

Ndege aina ya MH370 ilipotea mnamo mwezi Machi 2014 wakati iliopokuwa ikitoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing ikiwabeba abiria 239.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Picha ya mabaki ya ndege

Licha ya usakaji mkubwa wa mabaki hayo katika bahari ulioongozwa na Australia,ndege hiyo pamoja na abiria wake wote hawajapatikana.