Oscar Pistorius anyimwa ruhusa ya kukata rufaa

Oscar Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Oscar Pistorius alipatikana na kosa la mauaji Desemba

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amenyimwa ruhusa ya kukata rufaa uamuzi wa mahakama wa kumpata na hatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Mahakama ya Kikatiba ndiyo iliyotoa uamuzi huo, na ina maana sasa kwamba Pistorius atahukumiwa Aprili.

Pistorius alimuua Bi Steenkamp Februari 2013 baada ya kufyatua risasi mara nne kupitia mlango wa choo alimokuwa mpenzi huyo wake.

Uamuzi wa awali wa kumpata na kosa la kuua bila kukusudia ulibatilishwa Desemba mwaka sana na badala yake majaji wakampata na hatia ya mauaji.

Huwezi kusikiliza tena