Mwanafunzi wa Misri kufurushwa US baada ya kumtishia Trump

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Donald Trump

Mwanafunzi mmoja raia wa Misri anakabiliwa na makosa ya kurudishwa nyumbani kutoka Marekani baada ya kuchapisha katika mtandao wake wa Facebook kwamba yuko tayari kumuua mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican Donald Trump na dunia itamshukuru,kulingana na chombo cha habari cha AP.

Emadeldin Elsayed mwenye umri wa miaka 23,hakabiliwi na mashtaka ya uhalifu kufuatia ujumbe huo,lakini alikamatwa na mamlaka ya uhamiaji mwezi uliopita na atahojiwa ili kubaini iwapo atarudishwa nyumbani Misri.

Image caption Elsayed

Bwana Elsayed amesema aliandika ujumbe huo kwa sababu alikasirishwa na matamshi ya Trump kuhusu waislamu.

Amesema kuwa anajuta kuandika ujumbe huo na kwamba hakulenga kumuumiza mtu yeyote,AP imeongeza.