Twiga Stars kuivaa Zimbabwe kesho

Image caption Timu ya taifa ya Wanawake Twiga Stars

Timu ya taifa ya Tanzania ya wanawake Twiga Stars Ijumaa itashuka dimbani kuchuana na timu ya taifa ya wanawake ya Zimbabwe.

Mchezo huo ni wa kuwania kufuzu kwa fainali za michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake.

Mchezo huo utachezwa katika uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Waamuzi wa mchezo huo watakua ni Lidya Tafesse, akisaidiwa na Yehuzewdubizua Yehuw, Tsige Sisay, Woinshetkassaye Abera kutoka nchini Ethiopia, huku Kamisaa wa mchezo akiwa ni Geneviev Kanjika kutoka Jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo