Kilichomuua mwanawe Whitney Houston chatajwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bobbi Kristina

Mwanawe mwimbaji maarufu marehemu Whitney Houston alifariki baada ya kuzama majini pamoja na ulevi wa dawa za kulevya ,ripoti ya matibabu imebaini.

Marehemu Bobbi Kristina aliyekuwa na umri wa miaka 22 alifariki katika hospitali moja tarehe 26 mwezi Julai ,miezi sita baada ya kupatikana bila fahamu katika choo cha kuoga.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bobbi Kristina na mpenziwe

Ripoti ya matibabu ya Faulton County mjini Atlanta ilitoa taarifa baada ya kufanyiwa upasuaji na ukaguzi miezi saba baada ya kifo chake.

Jaji mmoja mjini Atlanta alitoa agizo siku ya Alhamisi la kuiweka wazi ripoti hiyo kufuatia ombi la vyombo vya habari.

Waliofanya uchunguzi huo wanasema kuwa walichunguza rekodi za matibabu za msichana huyo na stakhabadhi nyengine ili kubaini chanzo cha kifo cha mwanadada huyo wa Marekani.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mazishi ya Bobbi Kristina

Uchunguzi huo ulibaini kwamba matumizi ya bangi na pombe yalichangia katika kifo chake pamoja na dawa za kutibu wasiwasi.