Ashtakiwa kwa kulichoma gari la Dodi Fayed

Haki miliki ya picha PA
Image caption Binti mfalme Diana na aliyekuwa mpenziwe Dodi Fayed

Mtu mmoja raia wa Australia ametuhumiwa kulichoma gari moja aina ya Ferrari lililokuwa likimilikiwa na mapenziwe binti mfalme Diana wa Uingereza Dodi Fayed.

Raia huyo kutoka mji wa Melbourne pamoja na wanawake wawili walikamatwa siku ya Alhamisi ,miezi minne baada ya maafisa wa polisi kulipata gari hilo likichomeka ambalo lina thamani ya dola milioni 2.

Gari hilo ni miongoni mwa magari mawili yalioibwa kutoka kwa fundi mmoja.

Wanawake hao waliachiliwa bila kufunguliwa mashtaka ,lakini mtu huyo aliyejulikana na vyombo vya habari katika eneo hilo kama Kane Ridley,alikabiliwa na makosa mengi ikiwemo uchomaji.

Mahakama iliambiwa siku ya ijumaa kwamba Ridley,ambaye alizuiwa anaugua tatizo la kujiondoa katika utumizi wa mihadarati gerezani.

Magari hayo yanadaiwa kuibwa kwa dakika nne,baada ya wezi hao kuvunja mlango na kuingia katika nyumba iliokuwa na magari hayo huko Braeside.