Je, mwandishi wa al-Shabab Hassan Hanafi ni nani?

Image caption Hassan Hanafi

Mwandishi wa Somalia Hassan Hanafi alihukumiwa kifo kwa kupigwa risasi na mahakama ya Mogadishu siku ya Alhamisi baada ya kufanya njama na kundi la al-shabaa katika mauaji ya waandishi wenzake 5.

Hanafi alikuwa maarufu sana kwa wasikilizaji wengi wa redio nchini Somalia baada ya kujiunga na idhaa maarufu ya Quran FM kulingana na mwandishi wa BBC Abdinoor Aden.

Aliondoka mwaka 2006 ili kuwa mwanahabari wa mtandao wa Somali.

Baadae alijiunga na al-Shabab na kuanzisha afisi ya siri,iliokuwa ikichunguza habari na kumtishia ripota yeyote ambaye alizungumza dhidi ya al-shabab ama hata kuliangazia kundi hilo kwa njia mbaya.

Baadaye angemtaka mwandishi aliyelikosea kundi hilo kumfuata katika gari lake.

Wengine waliuawa papo hapo huku wengine wakikana na kulitoroka taifa hilo.